Kama huyu mtu angemfungulia mkewe mlango muda huu, (1:17am), hapo ningeamini ule msemo wa wanazengo kuwa kawekewa Limbwata
Yaani mwanamke timamu, unamuacha mumeo saa nne usiku wakati tayari mlikuwa mmekwishapanda kitandani, unashawishika na mshika masikio mwenzio, mnaambatana kwenda kwa jirani kwa kile mnachokiita Friday Party. Kwa dharau unalewa mpaka saa 7 hii, halafu unabaki ukilalama eti nilikuwa chumba cha jirani hapo pua na mdomo. Halafu unalalama eti mume anadharau, hataki kukufungulia mlango, saaaaad!
Alivyo kiburi karudi kwa rafiki yake kulala, yaani karudi kwenye party
Halafu kwenye party yenyewe kuna madume wawili, mmoja bachela, mwingine hana time na familia, halafu wote unaambiwa ni wachakataji holela. Anyway hayo mengine tuyaache, turudi kwa huyu mwanamke
Hivi huu ni uungwana kweli? Mumeo katoka kazini, kachoka, kakuemelea kila kitu mpaka vya kesho chaini. Karudi akiwa amejaa upwiru, wewe unamuacha unakwenda kwenye soga. Inasikitisha sana
Siku mkisikia Bwana Melki anatangaza ndoa na Bi Dazeti Mweusi kutoka Mkulanga, naombeni mnikate mashine
Inasikitisha, badilikeni! Nitawaletea mrejesho wa kilichoendelea itakapitimu asubuhi