tunaambiwa kuwa kabla ya kuanzishwa ukoloni barani afrika, walitumwa watu kwa ajili ya kufanya upelelezi katika bara la afrika. na kwa watu waliopata kusimuliwa na kusoma historia juu ya wapelezi, wengi hujiuliza ni kwa njia gani Wapelelezi hao walifanikiwa kuwasilana na waafrika?. kwani waafrika walikuwa wakitumia lugha zao za asili na wazungu pia walikuwa na lugha zao za asili. lakini ukweli ni kwamba Wazungu walipata shida sana walipokuja barani afrika kwa lengo la kupeleleza. Na walipokuwa wanakuja barani afrika, waliopaswakuja walikuwa wasomi wa hali ya juu hasa katika mambo ya kijamii na kijiografia. hivyo ilikuwa lahisi sana kwa wapelelezi hao kujua mambo mengi juu ya bara la afrika na watu wake kwa ujumla. na kikubwa zaidi wapelelezi wakishirikiana na Wamishionari, walifanikiwa kuwafundisha waaafrika wachache kwa haraka sana, kwa lengo la kupata watu watakao kuwa wanatumiaka kama Wakalimani. na hivyo ikawa kazi lahisi sana kwa wazungu kujua mambo mengi katika bara la afrika na kufanikiwa kuanzisha ukoloni barani Afrika. sasa picha hii inaonyesha namna wakoloni walivyokuwa wakiwasiliana na waafrika huku kukiwa na mwafrika mmoja ambaye alikuwa kama Mkalimani. Na inafafanuliwa kuwa waliokuwa wakitumika kama wakalimani ni wale watoto wa Machifu. na kitu kingine waafrika wengi walikuwa ni Wabantu, na lugha za kibantu ni nyingi sana na zilikuwa zinafanana. na hii pia iliongeza ufanisi mkubwa kwa wapelelezi hao kujua mambo mengi juu ya waafrika. kwa ujumla Wazungu walikuwa na uwezo mkubwa sana wa kutambua kile ambacho hawakukitambua kwani walitumia mbinu nyingi katika kutambua. na ndio maana hata leo mzungu akitaka kujua kitu ni lazima kutumia baadhi ya watu ambao wanakifahamu kitu hiko.