Mmh.. Jamani wanaume!! Huyu wangu amekuwa mkweli kaniambia nisiwaze suala la ndoa.. Kama nataka kuishi kwake niende muda wowote lakini mambo ya chereko chereko hataki kusikia...!
Hivi mtu unakuwa na mpenzi na anakwambia live kwamba hawezi kukuoa kwa baadae kwa sababu bado ana safari ndefu ya kutafuta maisha na bado anakwambia anakupenda. Hivi kweli kuna mapenzi ya kweli hapo, naombeni ushauri wana Jf.
Wakati anakuletea Muswada mbona hukutushirikisha? Umesha -sign, na sasa ndiyo unaona sheria yenyewwe haitekelezeki. Ndiyo unakuja kwetu. Acha hizo za Kikwete na Bunge lake weweee!!!!
Tatizo mnapenda kudanganywa, mkiambiwa ukweli masikio hayasikii macho hayaoni. Huyu kakuwekea mbele yako kuchagua kuendelea na uzinzi au kutafuta ambaye yuko tayari kukuoa. Yeye mbelembele atajua atakalofanya katika maisha yake akifanikiwa au akifeli kimaisha.