Kwa taratibu za Wizara ya Elimu siku hizi combination ya masomo ya msingi ni lazima uwe na minimum pass grade C meaning uwe na grand total points 9 minimum (anzia 3 points) kwa kwenda Advance Level. Kwa HGE wanapima C mbili za History na Geograpphy kama minimum entry na hesabu hapo upate at least C grade. Hivyo ninakushauri kuwa ni vyema uandikishe re-seat ili ukazane upate C za History na Geography. Kuna shule za Private zinakubali kupokea hizo D kwa makubaliano kuwa ni lazima ufanye re-seat upate C mbili hizo ili uweze qualify kufanya mtihani kidato cha 6. Kwako sasa tatizo una F ya Mathematics ambapo kwa masomo ya Business unatakiwa C. Hivyo basi kwa uamuzi mzuri ni vizuri sana usome combination ya pure arts ambayo hesabu siyo kigezo (HGL, HKL, HGK) kama unazo C grades. Shida hapo sijui Kiswahili na English ulipata ngapi ili upambane kupata C ya History.
Ila laiti tungelijua toka awali kuwa msingi wa mtu anayetaka kusoma huanzia Primary School ili apate Secondary nzuri theni Kidato cha nne ni kukazana upate grades za kukuwezesha kusonga kidato cha tano na cha tano unasoma kufa na kupona ili uweze kuingia Chuo Kikuu. Na kama una vision ya kusoma Masters na PhD ni lazima utie msuli wa kusoma sana ili chuo utoke na first degree nzuri ya First, Upper au better lower Second (chance ndogo) ili uweze kupenya Masters ambayo nayo ni lazima upige makasia upate first na Second classes as Phd Passport. Sasa tukishaharibu hatua moja jua kabisa hatua zinazofuata ni lazima mtu uanze kutapatapa sana na hapo maji yakishamwagika hayazoleki.
All the best.