katika vitabu vya dini imewekwa bayana ni wajibu wa wanachi wote kuheshimu mamlaka zilizowekwa kwani viongozi hao chombo cha Mungu kwetu wanadamu,
ROMANS13: Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu. 2 Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu. 3 Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu. 4 Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu. 5 Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri.
haijalishi kiongozi ana mapungufu kiasi gani kinachotakiwa ni kuheshimu mamlaka yake na kutumia busara katika kusahihisha makosa na mapungufu yake, tatizo letu sisi tunashindwa kwanza kuheshimu mamlaka, na vilevile badala ya kutumia busara katika kukosoa na kurekebisha makosa ya viongozi wetu tunatumia lugha zisizofaa, huku tukiwa sisi sisi ndio tunaomrudisha kiongozi husika nyuma katika juhudi anazozifanya katika kuleta maendeleo kwa watu wake. matusi, dharau, kejeli imekuwa ni sehemu kubwa ya kelele tunazozipiga kwa viongozi wetu kuliko ushauri, majadiliano yenye tija na mengineyo. tunashindwa kutambua ya kwamba yeye ndie tunayemtegemea na haipaswi kumrudisha nyuma, anaposhindwa kiongozi wananchi wanashindwa mara 10 zaidi yake. TUNAPIGA KELELE NYINGI KWA VIONGOZI WETU AMBAZO ZIMEJAA MATUSI ,KEJELI, LAWAMA, ambazo haziwezi zikatusaidia kama wananchi wa kawaida, ili viongozi wafanye kazi kwa misingi inayofaa ni lazima yale wanayoyasikia kutoka kwetu yawe ni yenye kujenga au yenye lengo la kusahihisha pale walipoteleza katika maamuzi yao. ingekuwa tunawapigia viongozi wetu kelel zenye tija nao wangejawa na hofu ya kutekeleza matakwa ya wananchi. viongozi nao ni binadamu kama binadamu wengine, hivyo wanahisia za hasira, majivuno, wivu n.k linapokuja suala la kiongozi kukosea halafu kila mmoja anamnyooshea kidole cha kejeli, kwa mara ya kwanza hujiskia vibaya ila hujipa moyo mara nyingine nitafanya vizuri zaidi, anapokosea mara ya pili na hali ikawa ni kama mara ya kwanza mambo hubadilika. tujifunze kuacha kunyoosha vidole vya kukejeli na kudharau na kuanza kunyoosha vidole vya kurekebisha na kushauri.