Heshima wakuu.
Ni kwamba mwaka jana wakati na install Kaspersky Internet Security (KIS) 2012 niliweka password Parental Control sasa nataka kuinstall KIS 2013, in the process of installation nikaambiwa niingize current password, bahati mbaya nimeisahau hiyo password, nimejaribu kuingiza password zote ninazokumbuka kuwa nilishazitumia zimekataa. Niliwatumia ombi Kaspersky Technical Support jinsi ya kureset au kuiondoa kabisa KIS 2012 lakini leo ni siku ya 4 nikicheck status bado inasema Waiting for reply from support team. KIS 2012 imeisha (expire) juzi, muda mwingi nakuwa online so naogopa virus wasije tumia nafasi hii kuishambulia computer na kupoteza data. Please naomba kwa yeyote anayejua jinsi ya kureset au kuiondoa kabisa Kaspersky Internet Security 2012
Natanguliza shukrani za dhati,