Kama unataka mapenzi ya kuchunana sina shida ila elewa wewe ni kama bidhaa niliyoinunu na nina madaraka yote juu yako. Unajua kabisa mahusiano yetu yamekaa kimaslahi, nakulipia kodi ya nyumba, mizinga kibao mara tairi za gari zimeisha, mdogo wangu anaolewa, nataka kufanya ka shopping kidogo mimi natoboka mifuko. Nikiwa na mademu wengini unakuwa mkali, kwani nani kasema tupo pamoja kwa ajili ya mapenzi? Upo kwangu kwa vijisenti ninavyokurushia rushia bila hivyo ungeshaondoka kitambo na mimi nipo kwako kwa ajili ya ngono, wewe ni mzuri sana kitandani na hata umbo na sura yako inavutia sana tu. Huwezi kunizuia kuwa na wanawake wengine, ingekuwa upo kwangu kwa mapenzi ya kweli hapo sawa, wivu wa nini wakati hapa ni ka ATM kako? Kingine utambue huruhusiwi kuwa na vibuzi vingine, haiwezekani mimi nihudumie wengine wafaidi, kama umekuwa ghali sana na sikidhi mahitaji yako sema uchape mwendo. Siku nikijua una vibuzi vingine nakata mfereji.
Chagua moja, kama unataka mapenzi ya kweli au ya kimaslahi, haiwezekani ukataka vyote na ukapata!