Heart Valve dysfunction

Mzee23

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
1,742
Reaction score
3,673
Nilizaliwa nikiwa na shida kwenye moyo (miaka ya 90), kwakuwa nilikulia kijijini, msaada wa matibabu kitaalamu haukuwepo. Wakati huo ilikuwa hasa kichomi nikifanya kazi ngumu au kukimbia kidogo na kuishiwa nguvu.. (sasa naelewa ni "exercise intolerance") baadaye kuanzia 2015 hivi hadi sasa ni kupumua pumzi haifiki mwisho("shortness of breath") na sasa imeongezeka hali ya kushtuka usiku kwa kukohoa mfululizo( "Paroxysmal nocturnal dyspnoea")

NOTE: najua majina ya hali hizo kitaalamu sababu nasoma mambo hayo(Afya) chuo na nataja ili nieleweke haraka kwa wataalamu!

Nimeshafanya vipimo vya moyo Echo,ECG mtaalam mmoja akaniambia sina shida ya moyo, mwingine mwaka jana akasema kuna valve moja imelegea.. ila kwenye tiba akadai ni shida ndogo sana na itapona akanipa Propranolol ila bado dalili nilizosema zinazidi kukua! na ganzi inanitesa pia kwasasa mikono na miguu..!

Hoja: kuna tiba (dawa) inaweza kurekebisha valve iliyolegea? Au kurekebishwa bila upasuaji wa moyo? Au nahitaji upasuaji?
Umri32
ME,
DOM.
 
Kama unaweza kujichanga upate referral ya kwenda Apollo India unaweza kuwekewa valve ya bandia.
Na vipi mwenye shida kwenye chembe ya moyo. Chembe ya moyo zimekakamaa tiba yake ni nini?
 
Heart Valve dysfunction hua inasababishwa na bacteria wa mafua, Tonsils na kikohozi so pindi wanapokua kwenye koo hua wanashuka na ukingia kwenye mishipa ya moyo na kushambulia Valves.

Mkuu jaribu kutumia sindano ya Penicillin benzathine (Penadur) kila mwezi itakusadia inaweza kua dozi hata ya miaka 5. Dawa hii inatibu bacteria mbalimbali mwilini so itakusadia pia Valve nyingine iliyobaki isishambuliwe.

All the best mate, Nakutakia uponywaji mwema kwa jina la Mungu
 
Pole sana ndugu yangu.
Najua hata kama ulikuwa hujasomea medical ukiwa na changamoto fulani unalazimika kuijua hata zaidi ya madaktari wenyewe, maana hata daktari asome vipi kama hajawahi kuumwa ugonjwa unaoumwa hata umweleze vipi hawezi kuyahisi maumivu na changamoto unazopitia.Ndio unakuta mtu akitoa tatizo lake mtu aliyesoma vi symptoms kwenye vijarida anaanza kukushauri mara fanya mazoezi, kunywa maji mengi, na longolongo kibao kumbe hajui lolote.

Kama una uwezo ndugu yangu mabingwa wa moyo ni India angalau doctor masau alikuwa anajitshidi kwa bongo ila ndio hivyo hakudumu
 
Kama unaweza kujichanga upate referral ya kwenda Apollo India unaweza kuwekewa valve ya bandia.

Nakuona kila siku unazidi kuwa mrembo tu au ndio mambo ya Cosmetics ??🤣🤣
 

lakini jinsi unavyouelezea huo ugonjwa wako it seems to me as if you, if not a physician, are a medical student !!.-- isiwe ni swali la mtihani au kuna mgonjwa kakutatiza mahali unatafuta msaada, 🤣🤣

Juu ya yote, pole sana mkuu na Mungu atakuponya, amiin.
 
Asante, kwenye vipimo gani wanaweza kuonekano hao viumbe? Ili uwe na uhakika kwanza kuwa wao ndio chanzo!
 
Hakika mkuu! Unajikuta bingwa kabisa wa ugonjwa wako kwa lazima!

India pesa ndugu hadi kujichanga kwelikweli!
 
Ukisumbuliwa na gonjwa flani serius kwa muda mrefu utajikuta bingwa wa ugonjwa huo bila kutarajia mkuu! Acha tu yasikukute
 
Asante, kwenye vipimo gani wanaweza kuonekano hao viumbe? Ili uwe na uhakika kwanza kuwa wao ndio chanzo!
Bacteria??? Nina uhakika wao ndio wanasababisha. Hakuna vipimo vya kuowaona hao bacteria ila hua tunaona madhara yake. Si unajua mafua, tonsils nk vyote hivyo vina bacteria? So it's proved kwamba Valve dysfunction hua inasababishwa na hao bacteria. Siongei hivi ili kufurahisha kijiwe bali kwakua najua maana nipo sekta hii mate
 
Asante sana nalifanyia kazi
 
Hii kitu imenisumbua tokea nikiwa mdogo. Ila nikiwa chuo ndio ilipamba moto, nilikuwa naendaga kwa Dr. Masau, kikubwa dawa za kutumia ni hizi propranolol. Sindano nazo husaidia ila sindano ni kali kupita maelezo. Mengine madaktari wataeleza
 
Hii kitu imenisumbua tokea nikiwa mdogo. Ila nikiwa chuo ndio ilipamba moto, nilikuwa naendaga kwa Dr. Masau, kikubwa dawa za kutumia ni hizi propranolol. Sindano nazo husaidia ila sindano ni kali kupita maelezo. Mengine madaktari wataeleza
Unakuwa huenjoi utoto kabisa!
Vipi kwasasa unaendeleaje?
Dr Masau alisema chanzo, tiba kabisa ya hii kitu ipo?
Uliwahi shauriwa kwenda India?
 
Unakuwa huenjoi utoto kabisa!
Vipi kwasasa unaendeleaje?
Dr Masau alisema chanzo, tiba kabisa ya hii kitu ipo?
Uliwahi shauriwa kwenda India?
Kwa totoz siyo shida sana, ila kipimo ni muhimu. Vyanzo vipo vingi ikiwa ni pamoja na kuridhi. Vipimo vilionyesha ni mild prolapse hivyo kulikuwa hakuna recommendation yoyote zaidi ya periodical reviews.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…