TOKA MAKTABA :
6 February 2020
Mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli, rais wa TLS atoa nondo kali:
Mfumo wa sheria za jinai ulioko sasa nchini Tanzania , hauna tofauti na sheria za kikoloni, zilizotumika kutia hofu wananchi ili watii amri za kikoloni bila kuhoji.
Kauli hiyo imetolewa na Dk. Rugemeleza Nshala, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), leo tarehe 6 Februari 2020, jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini.
Dk. Rugemeleza Nshala ameishauri serikali ya Rais John Magufuli kufanya mabadiliko ya sheria katika mfumo Haki Jinai, ili kuondoa sheria kandamizi zinazonyima watuhumiwa dhamana.
18 September 2021
Dr. Rugemeleza A.K Nshala, rais mstaafu wa Tanganyika Law Society TLS amesema mfumo wa Jinai Haki ( Criminal Justice System) wa nchini Tanzania unahitaji mabadiliko makubwa kwa kufumuliwa na uundwe upya ili kulinda haki za raia na watu . Azungumzia mazito kuhusu Nolle prosequi / kufutiwa...
Dr. Rugemeleza A.K Nshala, rais mstaafu wa Tanganyika Law Society TLS amesema mfumo wa Jinai Haki ( Criminal Justice System) wa nchini Tanzania unahitaji mabadiliko makubwa kwa kufumuliwa na uundwe upya ili kulinda haki za raia na watu .
Azungumzia mazito kuhusu
- Nolle prosequi / kufutiwa mashtaka bila kuelezwa sababu za msingi zaidi ya ofisi ya DPP kusema imeamua kutoendelea na mashtaka
- Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka DPP
- Makubaliano kati ya raia na kitu kinachotisha kikubwa yaani raia asiishitaki serikali akiachiwa pia asidai fidia
- Marekebisho ya sheria yanahitajika ili mahakama iweze kusikiliza haki ya dhamana na ikiwa inafaa mahakama ipewe mamlaka ya kumuachia mtuhumiwa wakati Polisi na waendesha mashtaka wakiwa wanaendelea kusaka ushahidi
- Watuhumiwa wengi wanaozea ndani ya mahabusu gerezani kwa muda mrefu wakati inadaiwa vyombo vinaendelea na upelelezi
- Mtuhumiwa siyo mhalifu mpaka hapo atakapo pata haki yake kwa kuhukumiwa na Mahakama.
- Hii ya mtuhumiwa kuhukumiwa na Polisi, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka au kiongozi yeyote ni uvunjifu wa haki za raia na katiba.
- Wenye jukumu la kurekebisha mfumo huu Jinai Haki, ni serikali iliyopo madarakani kwa kutumia wataalamu wake na bahati kuna wasomi bobezi waliopo ofisini , ni kama Mwanasheria Mkuu Jaji Dr. Feleshi, Waziri wa Sheria Prof. Palamagamba na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Wadau wengine kama TLS, Kituo cha Haki za Binadamu, Vyombo vya Habari na wananchi ni kupaza sauti na kupigia kelele mfumo huu mbovu wa Haki Jinai uliopo sasa hivi.
- Polisi hawawezi kulaumiwa, wao Polisi hawana jukumu lolote bali kupiga saluti na kutekeleza amri na sheria hii mbovu inayoendesha Mfumo Haki Jamii ( Criminal Justice System) kama wanavyoelekezwa na viongozi wanaowaongoza jeshini na wanasiasa serikalini.
- Watanzania tuamke toka dhamira zetu zilizo mfu, tupiganie haki hii wote kabisa bila kujali vyeo vyetu, vyama vya kisiasa, itikadi n.k
Rugemeleza Nshala, holds Doctor of Juridical Studies (S.J.D) from the Ivy league Harvard Law School. He holds a Bachelors of Laws Degree (LL.B) from the University of Dar es Salaam, Tanzania (his home country), which he obtained in 1993; the Masters of Laws Degree (LL.M) from Harvard Law School and Masters of Environmental Management (MEM) from Yale School of Forestry and Environmental Studies that he obtained in 1997 and 2007, respectively. Source :
Harvard African Development Conference
Haki Jinai / Criminal Justice System
SERIKALI YAJIPANGA KUBORESHA MFUMO WA HAKI JINAI
Imewekwa: Wednesday 15, June 2022
SERIKALI YAJIPANGA KUBORESHA MFUMO WA HAKI JINAI
Serikali imejipanga kuboresha Mfumo wa Haki Jinai nchini kwa kubaini changamoto na kupendekeza maboresho katika mnyororo mzima wa haki jinai. Hayo yamebainishwa katika Kikao kazi kilichoandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Wadau wa Haki jinai nchini. Kikao kazi hicho cha siku tano kimefunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu leo tarehe 13 Juni, 2022 Jijini Dodoma.
Dkt. Kazungu amewataka Wadau wa haki jinai kujadili changamoto zinazoukabili mnyororo mzima wa haki jinai na kupendekeza namna bora ya kuboresha mfumo huo ili kujenga mfumo madhubuti wa sheria unaoaminika na jamii katika utoaji haki.
Maoni yatakayotolewa katika kikao kazi hiki yatatumika kuboresha Andiko la Mapendekezo ya Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai Nchini kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 hadi 2026/27.
Aidha, Dkt. Kazungu amesema mabadiliko ya mfumo wa haki jinai yamekuja wakati muafaka kwani hayo yamekuwa moja ya maono ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro tangu alipoteuliwa kuongoza Wizara hiyo
Source :
https://www.sheria.go.tz/news/serikali-yajipanga-kuboresha-mfumo-wa-haki-jinai