Hapa kazi tu!!!

Champ

Senior Member
Joined
Aug 14, 2018
Posts
109
Reaction score
190
Mlozi wetu yu hai bado..... Unalipia king'amuzi uone tatu mzuka na biko aghalau ukishinda ujue, mara unasikia uliyemlipa amekatazwa kutoa huduma kwa sababu alikutoza kimakosa. Hapo umeibiwa mara 2: kulipia huduma ya bure na kulipia huduma pasipo kuipata.
Ulikuwa unanunua cement kwa Tshs10000, akaletwa Dangote ili ununue kwa Tshs6000 lakini sasa imekuwa 10000+6000.
Kasi hii ya kuwapigania wanyonge ikiendelea hivi kwa mara ya kwanza tutashuhudia masikini akifilisika!! [emoji22]
 
Hili suala la Vingamuzi kuonyesha TBC kutwa kucha linakera sana. Lkn vigezo na masharti kwenye kadi za hivi Vingamuzi kuna kipengele kinasema, WATOA HUDUMA WANAWEZA KUONDOA AMA KUWEKA CHANELI YOYOTE WAKATI WOWOTE. Naamin tulisain mikataba hiyo wakati wa kuunganishiwa huduma, lkn je ndio hawa mabwanyeye waigeuze fimbo kwa wanyonge kweli? Ngoja tuendelee kuangalia NatGeo mfurahie
 
Mm toka "Jiwe" ameingia madarakani simuelewagi Mnyonge anaemzungumzia ni yupi?Mnyonge anaempambania ni yupi? Anaishi nchi gani,yumo humu humu Tanzania au ni hadithi ya kusadikika?
 
Mm toka "Jiwe" ameingia madarakani simuelewagi Mnyonge anaemzungumzia ni yupi?Mnyonge anaempambania ni yupi? Anaishi nchi gani,yumo humu humu Tanzania au ni hadithi ya kusadikika?
Ni hadithi ya kusadikika mkuu, na huo ndo uhalisia wenyewe
 
Uongozi kipaji sio zawadi kama kushinda tatu mzuka. Tutaona mengi..
 
hiyo ni mbinu ya kuhakikisha TBC inapata wateja kwa nguvu, mbinu pekee ya kutoiangalia TBC kwa sasa ni kuzima TV na ndo mbinu ninayoitumia.
Ni bora kuangalia ukutani kuliko kuangalia hii TBC ya akina ryoba.
 
Bora ushinde na korean movie kuliko kuanagalia TBC
 
Wafanya biashara ni wajanja sana wanajua kuwa nchi (serikali) ipo busy na siasa za kuhama hama kama manyumbu wao wanafànya biashara ndo wanatumia mwanya huo kuongeza bei ya bidhaa na kutupiga wananchi.
 
hiyo ni mbinu ya kuhakikisha TBC inapata wateja kwa nguvu, mbinu pekee ya kutoiangalia TBC kwa sasa ni kuzima TV na ndo mbinu ninayoitumia.
Ni bora kuangalia ukutani kuliko kuangalia hii TBC ya akina ryoba.

Khaaa wewe mkurugenzi wa TBC akiona hii comment yako atatamani azimie [emoji38][emoji38]
 
Wafanya biashara ni wajanja sana wanajua kuwa nchi (serikali) ipo busy na siasa za kuhama hama kama manyumbu wao wanafànya biashara ndo wanatumia mwanya huo kuongeza bei ya bidhaa na kutupiga wananchi.
Hii ni kweli, ila ni wachache wataelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…