Nilikuwa naongea na rafiki yangu Mwingereza, akaniambia, "Tuwahamishe mkakae Uingereza na siasa yenu ya namna hii na uongozi wenu huu, na sisi tuje kukaa katika nchi hii yenye rasilimali hizi na siasa yetu kwa muda wa miaka 20 tu! Kwa miaka hiyo, maendeleo ya nchi yenu yatazudi Uingereza mara 10!" Nilifikiri sana. Kwa miaka hiyo huenda miundombinu ile, mazingira yale mifumo ile ya kijamii tungeharibu yote! Na huenda viongozi wetu wangeenda China kutafuta wawekezaji kuja Uingereza! Wasingereza wao wangetafuta namna ya kuingia ubia kwa miradi ya vitu kama gesi na dhahabu badala ya kupata mrahaba, Mabinde mazuri yenye mito ya kilimo yamgeendelezwa, bahari yetu ingekuwa ni mtaji elimu ingepewa msukumo mpya, wangeweka dira ya mapinduzi ya kilimo kwa muda mfupi ujao. ..na ...! Kweli hakuna nchi yenye siasa kama Tanzania!