Gyan akanusha kutoa kafara

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,356


Nahodha wa Ghana Asamoah Gyan amekana madai ya kuhusishwa na kifo cha rafiki yake ambaye ni rapa Castro, na kusema madai hayo ni ya kipumbavu.


Msanii huyo wa miaondoko ya kiafrika ambaye jina lake halisi ni Theophilus Tagoe alipotea akiwa na Asamoah Gyan mwezi Julai na mwili wake haujapatikana mpaka sasa.

Kupotea huko kwa kitatanishi kwa mwanamuziki huyo kunahusishwa na imani za kishirikina huku baadhi ya vyombo vya habari vya Ghana vikidai familia ya Gyan imemtoa ‘kafara’ mwanamuziki huyo.


Madai hayo yaliendelea zaidi mara baada ya kaka yake Gyan, Baffour Gyan kuhusika kumteka mwandishi ambaye alimhhoji Asamoah Gyan kuhusu tukio hilo la mauaji.


KabumbuWeb
 

Aaaaaa!!!!!kafara si imani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…