Habari wana jf,
Nina gari aina ya Toyota Mark II Grande (gx 110), nimeitumia kwa zaidi ya miaka minne sasa na hali yake sio mbaya sana japo inahitaji marekebisho kidogo kwenye tairi za nyuma( kubadilisha tu ball joints).
Nimefikiria kuiuza lakini changamoto za wanunuzi na usumbufu wa kila aina sitaki kabisa, hivyo kwa dhati hii gari nitaiacha na nitaitoa bure kabisa kwa yeyote anaehitaji.
Kwa nini sasa? Kwa sababu nina safari ya kwenda mbali kidogo mwezi huu mwishoni na kurudi yaweza kuwa miaka minne au mitano ijayo.
Sent using
Jamii Forums mobile app