Simu yangu ina mawenge haya.
Ikiwa kwenye lock mtu akipiga nikipokea inazima na kuwaka.
Nikipiga simu upande wa pili ukipokea simu inazima na kuwaka.
Nikiwa kwenye menu nikishika icon ya app ili niwe kama naibadilisha hapo ilipo simu inawaka na kuzima.
Nikaamua niiflash. Fundi akasema bootloader ipo locked, lakini tukiwa tunaendelea na zoezi la kuunlock akaona betri langu ni chenga.
Akaniambia nibadilishe betri pengine ndiyo shida.
Badala ya kubadilisha betri mi nataka mashine nzima nihamishie tu hii display yangu.