Sababu inayofanya vijana wengi waangukie kwenye anasa, ni kuyaishi maisha ya kufikirika.
Kupenda kazi za aina moja, unakuta Kila mmoja anataka kazi ya kutumia computer, yaani hawataki kabisa kukimbilia shambani, utakuta vijistudio vingi mitaani, music production uchwara, kuuza CD, sijui kuingiza nyimbo kwa flash, akijitahidi sana kafungua kijisaloon mtaani, Hadi unashangaa hili frem analipaje, Kodi alikopanga je? vipi kuhusu mahitaji mengine.
Pia unaweza kukuta vijana wapo vijiweni wanapiga stori za magari makali, Mara BMW mara sijui Alphard, yaani mtu anazungumza vitu vya million hamsini huko ikiwa laki tano hajawahi kushika.mara sijui nani ana hela kumzidi nani, yaani dah
Viwanja vya bata, unakuta kijana analeta maisha ya maigizo kuingia kumbi kubwa za starehe wakati Hana uwezo huo, kinachofuata ni kujiingiza kwenye utapeli na wizi ili aendane na maisha anayolazimisha.
Kutamani warembo wakali
Hapa napo Kuna tatizo kubwa sana, hasa ukizingatia mambo ya mitandao,kijana anajukuta anatamani mwanamke ambaye si saizi yake kabisa kuanzia muonekano, Elimu, ushawishi na hata umri, mwisho wa siku badala ya kutongoza , anatongozwa yeye na jimama, huku akipewa vizawadi vidogovidogo kama simu, cheni na vijinguo vya kubana, na akimakizwa kabisa atapewa Subaru, IST sijui Brevis
Hivyo kijana kama huyu huwezi kumfanyisha kazi za kufyatua matofali, saidia fundi, na vinginevyo.
Shida inakuja akiachwa ndiyo anaangukia kwenye ulevi, unga na vingine vya hovyo.
Ndoto za kuzamia ughaibuni,
Kijana anashindwa kutumia Elimu yake aliyoipata shuleni au chuoni mwisho wa siku, anakata tamaa maana maisha nayo hayataki mikato ya hivyo.