Feedback: Aliyeninyima namba na kunipa email

Michael Ngusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2014
Posts
1,637
Reaction score
463
Mwenzenu nimelala naomba pakuche ili ikajulikane kama nitafanikisha kuchukua mamba, maana kupitia calls, text, whatsapp n.k. ni rahisi kumvua sato.

Ile nimeingia tu nikapokelewa na booonge la smile kutoka kwny desk yake hadi nikajihisi "now this is being exaggirated!" Akanipa hi, nikaitika, "karibu sana, umeamka poa?" Nikasema poa kabisa.

Baada ya kazi natoka nje simuoni kumbe kajiegesha kwa mbali ili atumie wife ya bure eneo hilo, nikasogea."I want to leave", "hah why soon?" Nikasema "una muda sasa hivi nikufanyie photography?"

Akakurupuka "yeah nisimame wapi, ee huku, au huku!" Nikapiga picha kichwani laiti hayo maneno yangekuwa yanatamkwa kitandani"nikurambe wapi, hapa au huku!" anyway, nikaanza kazi.

Ghafla akaanza kuita mabeste zake nikashangaa nimekuwa mpiga picha wa kundi kubwa kazi yao kuchange location tu mpaka jasho linanitoka, nikasema hii haina tofauti na kwenda na Bar kisha kuja na mashostito wake.

Baada ya shughuli kuisha nikafanya tangazo "mwenye kunipa namba ili nimrushie kwa whatsapp! Kila mtu mimi mimi mimi, kazi yangu kunote tu, nikafika kwake "enhe, namba "si nilikupa email!" kidogo nianguke.
 
Hivi wewe na Aunt ezakiel ni damu moja
 
Mkuu leo ndo siku yako ya kumaliza huo mpango..we jitose kiume tu..if things goes wrong.. Jst tell her it was a prank..since 2day is April fool..
 
duuuh mkuu!! hiv uko serious au unafanya cku tu? maana umeniacha hoi kwa kicheko!!
so what next...!!!!?
 
Haaa! haaa! haaa! haaa! haaa! haaa! haaaaaaaa! Nimechekaje leo? Adi nimesahau nilichotaka kuandka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…