Miongoni mwa mboga za majani ninazopenda ni pamoja na tembele, leo ngoja niwashirikishe jinsi ya kuyapika matembele.
Pishi hili ni kwa wale wenye Maisha ya kawaida kabisa ambao tunapika bila vipimo (tunakadiria lakini msosi unakuwa mtamu balaa).
Mahitaji:
Matembele mafungu mawili ( hapa inategemea na mahitaji)
Nyanya tatu
Kitunguu cha wastani kimoja
Kariti moja( sio lazima sana)
Hoho( ukipenda sio lazima sana)
Mafuta kiasi
Chumvi kiasi
Jinsi ya kutayarisha.
Chukua matembele yako yachambue vizuri kutoa vinyuzi kwenye mikia yake kwa kuvunja mkia wake na kuvuta kile kivyuzi kwa kuwa huwa yanakua magumu kama usipotoa.
Waweza kuyaweka juani yanyauke kidogo kama ukipenda sio lazima sana(mimi hupendelea yaliyonyauka)
Naipenda mboga pia, ila kuwe na dagaa au samaki pembeni, Kuna matembele makavu yanachanganywa na dagaa na karanga alooo kwa wali tamu sana, Nimekumbuka nyumbani ghafla,
[emoji39][emoji1786]
Matembele, majani ya maboga ni mboga nazopenda sana na kupika mara kwa mara.
Kuna mboga inaitwa "mashasha" sijui mashona nguo nilikula juzi kwa mara ya kwanza aiseeee tamu sana nayo.
Nitajifunza mapishi yake.