Kuna siku niliona bandiko humu JF likisema wanaotaka kupakua facebook na kutumia vyema kwenye Android kirahisi iliwekwa link (kiambatanisho) nami sikujali kwakuwa wakati huo nilikuwa natumia blackberry ila sasa nasikitika coz natafuta link Ile sijaona, Lakini kubwa nimegundua facebook kwenye simu yangu ya android ni ovyo kuliko maelezo Yaani naona haina uwezo hata kuifikia jamiiforums app kwa ubora kwanza iko slow utadhani ninafungua mobile web na sio app Lakini kubwa siwezi kusave Picha hata zangu mwenyewe kwenye sds memory kitu ambacho jamiiforums wametegua Tatizo Hilo. Nimetumia facebook kwenye blackberry Nokia na simu tofauti hata zisizo na 3g sijaona Tatizo kubwa la utumiaji wa app ya facebook kama ilivyokuwa kwenye Android. Kwangu mpaka sasa Jamiiforums ni bora kuliko facebook kwenye simu ya android, sijui wewe maoni yako.