Everything happens for a reason

jf user

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2018
Posts
777
Reaction score
625
Kisayansi tunasema ili kitu kisogee basi lazima nguvu ya kukisogeza itumike.
Hii ina maana kuwa kitu kitaendelea kuwa hapo hapo labda kitasogea iwapo itatokea nguvu ya kukisogeza.

The same applied kuna vitu vinatokea maishani tunabaki tukijiuliza kwanini vimetokea? iweje wakati tupo na akili zetu timamu tunafanya vitu ambavyo kwa akili zetu hatuwezi vifanya? Au kwanini MUNGU kanipa kitu nisichokiweza au nisichokitaka kumbe ndugu yangu upo kwenye mapito na eneo ulilopo ni njia tuu ya mpito ya kukutoa sehemu moja kukufikisha sehemu nyingine.

MUNGU hakosei daima tuache kumlaumu MUNGU na kumsahihisha japo vitu vingine vinakera kwa sababu vimewahi nitokea personally ila nilivumilia na sasa naona matunda yake.
Maandiko yanasema atakae vumilia mpaka mwisho ndie atakae okolewa.
Stay positive siku zote.. avoid negativity kwenye maisha yako mambo yako yatakua okee siku zote.

Kama binadamu ambao ni wapitaji hapa duniani sio vibaya kusaidiana na kukumbushana mambo kadhaa ya kimaisha.
MUNGU awe nanyi.
 
Kuna situation napitia sasa kwenye maisha yangu, mpaka nimejiuliza kwa nini mimi? Nimekosea wapi? nahisi umenisema mimi kabisa,,,Asante.
 
Na tunapopitia katika hali ya changamoto nyingi ni vyema kumshirikisha Mungu na kumuuliza Mungu ni nini unapenda nijifunze katika hali hii ninayopitia?
Hakika yawezekana utapata majibu mengi kama ;
1, kuna wengi wanapitia njia pengine ngumu zaidi yako hivyo hauko peke yako
2, kutokana na shida ulizonazo faraja ni muhimu hivyo nawe utakuwa mtu wa kuwafariji wenye uhitaji
3, moyo wa kutoa msaada wa hali na mali hata kwa kile kidogo ulichojaaliwa
Hivyo utamshukuru Mungu nasi kumlaumu.
 
Umesema vyema, tuwe wavumilivu wenye tafakuri chanya ktk maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…