Habari za usiku wana jamii forum.
Mungu ni mwema nashukuru kwa uzima na afya. Kwa wagonjwa kama ommy dimpoz pole sana,msijali mtapona.Nakukubali sana ommy dimpoz kwa pozi, mijimbo yako kama wanjera,me and you,tupogo,ndagushima,nani kama mama bado naisikiliza hadi leo..Ninayo kwenye pc yangu na kila alhamis lazima nipige oldiz za bongo flava,kwenye playlist wewe,ali kiba (yooooh),lady jaydee na mwanafa ni ma all time favorite bongo flava artist.pamoja na dimondo nyimbo zake za kale.
Anyway,j3 baada ya kazi nilikwenda ARISA kuna shost yangu anafanya kazi pale.Ni geologist yeye.Kuna wateja walikuwa wanahitaji assistance na kufanya logistics flan so akanicall,tukakutana kujadil aone nawasaidia vipi halafu na yeye namtoa vipi kabla hajanikutanisha nao. (Siwajua mjini hapa ukitaka kula lazima uliwe hahahah).
Tukaonana,tukaagiza chakula na vinywaji ,tukawa tunakula huku tukiendelea na mazungumzo.Kama baada ya dk 45 wakaja wanaume wawili,wakaketi meza ya jirani na sisi.Kwa mazungumzo yangu nilijuaguess ni walimu pale.Bwana weeh sikio halina kiwambo wakati naamka kwenda msalani nikasikia,mmoja akimwambia mwenzake ,fulani bwana kashamaliza Phd yake.Amerudi nchini sasa anatafuta kazi.Looh nikaingia zangu wash room halafu nikacheka sana.Kwani niliwaza mtu amemaliza PhD then anatafuta kazi?Au aliunga kusoma from mwanzo to PhD then karud anatafuta kazi?Au Anataka kubadili kazi?
Anyways tunasafari ndefu sana katika kubadili mfumo wetu wa elimu.
Sent using
Jamii Forums mobile app