HUWEZI KUPANDA MBEGU MBOVU UKAVUNA MAZAO BORA , TUMECHAGUA KUZIMALIZA SHULE ZA SERIKALI.
A: Shule za serikali zinaendeshwa kisiasa kuwafurahisha wapiga kura .
1. Elimu bure kila mwezi billion 18 halafu hakuna pesa ya kuandaa mitihani, hakuna pesa ya vifaa vya kujifunzia, hakuna maabara,
2. Wanasiasa ndiyo wasemaji wa mwisho , maDC, RC, maDAS, madiwani, wabunge wanafanya ziara za kushughulikia walimu badala ya kushughulikia matatizo ya walimu
3. Darasa la saba wanafaulu wote mpaka wasiojua kusoma na kuandika, kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne ni bure bure hakuna mitihani ya kupanda
4. Wanasiasa wamepandikiza ujinga kwa wazazi walaumu walimu badala ya kushirikiana nao kusaidia watoto/wanafunzi
5. Syllabus zinabadilishwa na wanasiasa walimu wa shule za serikali wanapewa wazifanyie kazi bila mafunzo yeyote
6. Watoto wa shule za serikali wazazi hawana habari nao kazi kubeti, kucheza vituko, kukariri bongoflava na kuwinda walimu, ni maarufu kumfukuza mtoto asiye na nidhamu muache mpaka ahitimu.
B: Shule za private zinaendeshwa kitaalamu
1. Elimu bora yenye gharama, vitabu vingi , walimu wanalipwa vizuri, maabara nzuri , chakula safi , mabweni safi , mitihani mingi , yaani matumizi ya pesa yenye tija.
2. Wanasiasa marufuku kupeleka porojo zao kwanza watoto wao wapo huko lazima heshima itawale, siyo rahisi mwalimu wa private kuingiliwa na Dc, RC, DAS, diwani, mbunge kwenye mambo ya professional
3. Ni marufuku kupokea kilaza hata kama darasa la saba mtoto amefaulu lazima apimwe upya na kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne kuna mitihani ya mchujo, private siyo sehemu ya kilaza kabisa vilaza peleka shule za kata
4. Wanasiasa hawana nafasi ya kuchonganisha wazazi na walimu wa private yaani shule za private walimu na wazazi ni kitu kimoja wanafunzi/watoto wanatazamwa pamoja tena ushirikiano wao umetukuka... Hapa wazazi wengi ni wanasiasa kwa hiyo ni wakarimu kwa walimu wa private si wajua tena private ndiyo watoto wao walipo.
5. Syllabus zikibadilishwa mapema walimu wanapata mafunzo tena private nadhani ndiyo wanaanza kupata nakala za mabadiliko walimu wapo updates kweli kweli maana private hakuna kubana pesa , pesa zinatumika kwa tija
6.Watoto wa private wazazi wapo nao karibu yaani tabia za kishenzi hakuna sijui kubeti, kucheza viduku, kukariri bongoflava wala maana wazazi wanatoa pesa zao nyingi hawana mchezo mchezo kwanza mtoto asiye na nidhamu marufuku lazima atimuliwe sasa mzazi gani yupo tayari mtoto atimuliwe Milioni zake kumi sipotee bure .
NB : Acha wanasiasa wafanye watakavyo mpaka kwenye mambo muhimu yenye matokeo vizazi na vizazi, nadhani baada ya miaka kadhaa watu Wakurugenzi wa mashirika, wanasheria, madaktari, na wataalam wengine watakuwa watoto wa matajiri na watoto wa wanasiasa waliopata elimu bora yenye malipo yenye tija
Viongozi pitisheni jicho la huruma kwa watoto wa watanzania wenzenu nao wanapenda kufaulu siyo kuhitimu tu !!!!
ELIMU BURE