Mkolosai2020
Member
- Aug 11, 2022
- 22
- 31
Ila dhana ya EDUCATION FOR SELF RELIANCE aliomdoka nayo NyerereElimu yetu inafundisha watu kuwa woga
Kabisa, wasomi kwa sasa ni title tu siyo ELIMUUmaskini wa akili,umaskini wa chakula ,uwoga Kwa hiyo Bora liende nchi inaongozwa na kipofu ukiamka hili,kesho hili!
Tabia za kasuku ni kurudia kile kimesemwa lakini haelewi maana yake na hakumbuki tenakuwa amesema niniUkasuku ndio uchawa?
Nmekuelewa mkuuTabia za kasuku ni kurudia kile kimesemwa lakini haelewi maana yake na hakumbuki tenakuwa amesema nini
uoga wako ndio umaskini wako 🐒Miaka ya hivi karibuni hususani miaka ya kuanzia 2010 mpaka sasa kumekuwa na utamaduni wa kusifia sana wakuu wa nchi badala ya kuleta hoja zitakazo ibua sifa au kuelezea utendaji kazi halisi wa hawa watawala ama viongozi.
Binafsi nikijaribu kuangalia historia ya nchi yetu (TANZANIA) naona kama miaka ya sasa wasomi ni wengi ukilinganisha na miaka ya 1960s - 1990s.
Kusifia viongozi kuwaabudu na kuwanyenyekea kupita kiasi kumeibuka kwa wingi kipindi ambacho wasomi ni wengi sana ambapo karibia kila familia ama ukoo yupo mmoja aliyesoma chuo kikuu.
Yaani hakuna hoja italetwa bila kuanza na kupongeza fulani. Hata maeneo ambako hawahusiki hususani misibani, makanisani na misikitini lakini wasomi wetu wanasiasa huanza kwa kusifia tu.
Najiuliza maswali haya
1. Wasomi wetu wamejaa ukasuku kwaajili ya kupata teuzi?
2. Elimu ya sasa na zamani kuna tofauti gani hapa katikati ingali vyuo ni vilevile?
3. Kwani kiongozi kutekeleza mradi fulani siyo wajibu wake inakuja kama bahati mpaka apongezwe ndio atapata motisha ya kutekeleza zaidi?
4. Viongozi hawaelewi wajibu wao?