Dunia ni kama gari wenzangu......

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
614
Reaction score
322
Hii dunia ni gari yaweza ikapinduka.
Usione ufahari kulala ukiamka.
Elewa maisha safari haitaacha mashaka.
Wako wapi matajiri walio wakisifika.
Nyumba zao makaburi wala hawakuridhika.
Ni nyumba yenye hatari na walinzi malaika,
niwalinzi majasiri kwa Allah wamesifika,
ikiwa wewe jeuri yatakufika mashaka
Jee? uko tayari adhabu kuziepuka ?
Ikiwa upo tayari jitahidi kuamka!
uswali alfajiri udumishe hadi Isha.
Huu wangu ushauri mimi dhima naepuka
(WABILAH TAWFIQ)
 
Dunia kama iko hivo usikatae kushuka
+
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…