Nilifundishwa utotoni kuwa niwaheshimu watu wote lakini hata siku moja nisiwadharau ama kuwabeza watu wenye vyeo ama mamlaka, wenye fedha zao ama matajiri na wenye elimu yao.
Prof Muhongo ambaye siku hizi kajipatia umaarufu kwa kuitwa Muongo kwa kauli zake mbalimbali za uongo bungeni na kwenye majukwaa ya hadhara. Amewahi kuwadanganya wabunge na wananchi kwa ujumla kwamba hakutotokea mgao wa umeme tena. leo hii kuna mgao nchi nzima na bei ya umeme imepandishwa huku Naibu wake Simbachawene akitukebehi watanzania kwa kutuambia kuwa asiyetaka umeme aache na mbadala wake atumie kibatari! Muhongo ama 'Muongo' alipofikishwa kwenye kamati ya bunge ya maadili alitoa machozi na kuwaomba wajumbe wamsamehe na kwamba hatorudia tena kwa kuwa alidanganywa na wasaidizi wake.
Leo hii, pamoja na heshima niliyonayo kwa wasomi napata taabu sana kumuamini tena 'msomi' huyu kwa vile nahisi kama anadanganya tu na kwamba kila anachooongea hana uhakika nacho sana na kuna uwezekano mkubwa sana akawa anadanganya tena. Ukimuona anavyoongea kwa authority huwezi amini kama huyu 'msomi' anaweza kuwa anadanganya.
Tajiri Mengi naye sitaki kumtetea maana naye amekuwa akilia lia sana kuonewa lakini kumbe inasemekana naye anataka vitalu vya gesi. Pamoja na heshima niliyonayo kwa tajiri huyu napata mashaka sana na nia yake ya kutaka kuutumia vibaya uzalendo wa uzawa kujipatia mali yeye binafsi. Nakumbukia kwenye lile la Kilimanjaro Hotel, ambapo aliutumia sana uzawa wake kiasi ambacho mpaka leo hii watu wengine tunapata mashaka kama hii yake nayo si staili nyingine tu ya kutaka kutulaghai kwa kigezo cha uzawa kumbe ni mjasiriamali kazini?
Hawa watu wa aina ya 'msomi' Muongo na 'tajiri' Mengi ni wa kuwa nao makini sana. Utajuaje kuwa sasa ni wazalendo na wanamaaanisha wanachokisema? Ama wana nia zilizojificha moyoni?