DODOMA: Daladala zagoma kupinga manyanyaso

Don san tan

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2015
Posts
575
Reaction score
443
​

Zaidi ya mabasi 70 ya daladala yanayosafirisha abiria katika baadhi ya njia za manispaa ya Dodoma, yamegoma kutoa huduma kwa siku nzima ya leo.

Daladala hizo zinazotoa huduma kati ya Jamatini na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) pamoja na Jamatini na Veyula, zilisimamisha huduma zake kwa siku nzima ya leo zikipinga manyanyaso kutoka kwa askari wa usalama barabarani.

Baadhi ya madereva wa mabasi hayo, wamesema wamechoshwa na manyanyaso kutoka kwa askari hao kwa vitendo vyao vya kuwakamata kiuonevu.

Wamesema sababu kubwa ya mgomo wao ni rushwa na manyanyaso wanayofanyiwa na baadhi ya askari hao wa usalama barabarani.

​

Hata hivyo, akijibu malalamiko ya madereva hao, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Dodoma, Marisone Mwakyoma, amesema sheria zipo wazi kama kuna mtu anaombwa rushwa na kutoa, wote wana makosa kwa sababu zipo ngazi za kuripoti matukio hayo.

Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) mkoa wa Dodoma, Conrad Shio, amesema baada ya kutokea kwa mgomo huo waliweza kutoa kibali kwa magari mengine kuweza kubeba abiria wasipate shida ya usafiri.


Chanzo: EATV
 
Hili suala la rushwa viongozi huwa wanaongea kama vile kila mtu ni kiongozi, ni kwa vile hajapitia shida za madareva na madereva siyo wajinga mpaka wagome ujue wamechoka kweli. Tutafute ufumbuzi wa tatizo badala ya kukimbilia kuripoti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…