KARIBU SANA,UKAWA! Tunawakaribisha wote waliotambua kuwa kupitia UKAWA,Tanzania itaweza kukuwa kiuchumi siyo tu uchumi wa Taifa bali pia uchumi wa mtu mmoja mmoja na hatimaye kuondokana na lindi la umasikini. Hakuna mtu yeyote katika nchi hii asiyejua kwamba Tanzania tuna rasilimali za kutosha,lakini bado wananchi ni masikini sana. Tatizo tumekosa usimamizi bora wa rasilimali zetu. Sina maana kwamba tangu uhuru nchi haina maendeleo kiuchumi,la hasha; Hakika tunapotaka kupima maendeleo kiuchumi lazima tuangalie muda na rasilimali zilizopo,yawezekana kama pangekuwa na usimamizi mzuri na matumizi thabiti ya resources zetu tangu mwaka 1961 mpaka sasa tungepiga hatua kubwa kiuchumi zaidi ya hapa tulipo.
NYOTE MNAKARIBISHWA