Kila Binadamu hakosi SIRI, kuna siri ya Familia pekee, Siri ya Marafiki pekee, kuna Siri ya wewe na Mkeo, na SIRI yako mwenyewe!!. Ijapokuwa watu husema Siri isizidi watu wawili, hata zaidi waeza weka siri. Jambo kubwa kujiuliza, ni mwenye kupewa siri ataweza kuweka Siri??, kama si mtu wa kuweka siri ama mtu domo kaya kuna hatari ya kumwaga siri.
Wewe kama mwanaume, uta-amua siri utakazo mweleza mchumba/mkeo ikitegemea unavyo muona mwenzio na sio kwa wakati mmoja, na sio kila siri, umpe!!!. Kuna siri ambazo mtu huenda nazo kaburini!!