MTANGAZAJI wa Redio Times FM, Khadija Shaibu Dida amesema siku zote anapokuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi akigundua mtu wake ana date na mwanamke mwingine, kamwe hatathubutu kugombea bwana ila atanawa mikono.
Akibonga na paparazi wetu hivi karibuni Dida alisema , hakuna kitu ambacho kwake anaona ni cha kipuuzi kama kugombea penzi , kwa kuwa mtu anapokusaliti ni wazi upendo wake umehamia kwa mtu mwingine hivyo hawezi kujing ang aniza.
Nawashangaa sana wasichana wanaokosa kazi ya kufanya kwa kuanza kuwagombea wanaume, wengine wanadundana hadi kutoana manundu, hivi nigombee bwana kwani wanaume wameisha? Mimi nikimkuta mtu wangu yupo na mtu mwingine wala sijishughulishi, nachukua hamsini zangu, alisema Dida