Saa hizi saa sita na dakika 14,kwikwi inanitesa balaa,sijui ntafikaje asubuhi.
Pole,
Kuna sababu za muda mfupi na muda mrefu zinazosababisha kwikwi. Kuna sababu zinazoweza kuondoka zenyewe na kuna zinazohitaji kufanyiwa tiba ili kuondoa kwikwi na sababu yake.
A: Kwikwi ya muda mfupi/chini ya saa 6, unaweza kutumia njia za asili kama:
1: kunywa maji
2: kuacha kupumua kwa muda/ kushikilia pumzi kwa muda.
3: kuweka maji kwenye beseni na kuweka uso wako.
4: kufanya kama unasukutua maji kwenye koo/giggling nk.
Njia ya asili inaposhindikana ni vyema kufika kituo cha afya ambapo utapata kuangaliwa vyema na kupewa tiba halisi na ikiwezekana kupewa tiba ya chanzo cha kwikwi.
B: Kwa kwikwi ya muda mrefu/zaidi ya saa sita au inayokufanya ushindwe kula/kupumua/kulala au iliyoshindikana kuondoka kwa tiba ya asili:
Ni vyema kufika hospitali na kuangaliwa ni nini chaweza kuwa ni sababu. Ni muhimu ili pamoja na tiba ya msingi, pia utahitaji kufanyiwa tiba ya chanzo cha kwikwi. Kwikwi ya muda mrefu yaweza kuwa ni ishara ya tatizo jingine muhimu kutatuliwa kama:
1: shida ya figo
2: shida ya sikio
3: shida ya njia ya chakula
4: shida ya ubongo
5: shida ya madini mwilini nk.
Kuna dawa za aina mbalimbali ambazo huweza kuzuia au kuondoa kwikwi. Dawa hizi zimekuwa zikitumika pia kwa kazi nyingine kama:
1: kulainisha misuli
2: kuzuia kutapika
NB: Dawa na utaratibu wa kuondoa kwikwi upo, ila suala kuu ni kuzingatia mwenendo mzima wa kwikwi na hali ya mgonjwa husika.