*Hekima tulizopewa tukishindwa kuzitumia basi ujinga utaziba pengo*
*Yamkini maisha yako yangekuwa sinema Leo ungewa sehemu ya ngapi usiseme uongo*
*Ninapowaza kupunguza mawazo kwa kukaa kimya nakosea kidogo*
*Wapo wa kuwaheshimu na kuwapenda lakini wapo wa kuwapa kisogo*
*Akili yako itakapokutuma Fanya jambo lisiwe wimbo fanya ila ukiyumba kwako ni pigo*
*Wapo wanaotupenda ingawa hatujui, mawazo yakiwa mgando utawachukia kwa kishindo*
*Anaekupenda kweli hata mkigombana na mkatengana hapendi kusikia unateseka huo ndo upendo*
*Matatizo tuliyonayo yanafanya tujifunze mengi pamoja na uzalendo*
*Yawezekana huna kitu lakini we ni tajiri wa mipango vingine weka kando*
*Mungu tusamehe kwa yote tufanyayo yasiyo ya kibiashara na mapenzi kimagendo*
*Ni majira gani haya watu huteseka namna hii hata nikisoma maandiko sioni namna ya kusafisha chumvi*
*Njaa iliyoambatana na misiba ni ujumbe gani huu wanashindwa kutafakari hadi wazee wenye mvi*
*Tunafahamu magonjwa ni barua kwamba kuna mahali umekosea haya nayo ni vipi mpaka watakatifu wawe walevi*
*Jamii inapata utata watoto wa chekechea wanopokuwa wajanja kujihusisha na malavidavi*
*Sipati picha bunduki inapokwama katikati ya mapigano kifo ntakiepuka vipi*
*Niwaambie nini watu wangu moyoni tuwe wasafi tusijaze makapi*
*Uzee utakapokuita ndipo utagundua starehe za ujana zilikuponza ulipaswa kuvaa nepi*
*inauma kuona mabaya wakati huna nguvu ya kuyabadilidha kuwa mazuri*
*Basi bwana wekeni mikakati mtapendwa kwa harakati lakini msitegemee ufahari*
Hili ni darasa huru hakika