Huu mjadala mzuri sana na mimi ningependa nishiriki. Swala la kuwa na customer wengi sio issue kabisa, huyu mdada alitakiwa ampe huyu client muda wote unaohitajika kupata suluhu ya swala lake. Swala la kuwa na wateja wengi halimuhusu mteja, kampuni kwa kujua flow ya client wao wangetakiwa kuwa na staffing ya kutosha kukidhi haja zao. Kumwambia mteja akate ticket nyingine ni kumbebesha tatizo mteja na dhana nzima ya mteja ni mfalme imezikwa. Kampuni hii ilitakiwa impe mteja wake benefit of doubt, kwanza kwa kuomba aonyeshwe hiyo ref number na automated communication kwa kuangalia message iliyotoka fastjet. Tatizo sisi kama wateja pia hatujui haki zetu, katika nchi ambazo vyama vya walaji vinatambulika na vina nguvu, huyu bwana angedai usumbufu na embarassment na kampuni ingemlipa. Hili sio tatizo la fastjet tu, ni kwa makampuni mengi sana ya hapa nchini, hata zile za nje zinazofanya vizuri duniani zikija hapa kwa kujua kuwa watanzania ni wajinga, zinafanya shaghala baghala, tunachotakiwa kwa sasa ni kujiunga kwa wingi na vyama vya walaji ili kuvipa nguvu. Leo hii angalia kampuni za simu zinavyofanya uharo, unaweka kabang haiingii ukiwafuata hadith ndefu, uki scratch voucher ukaharibu huoni namba unaenda kwao wanakujazisha makaratasikibao na kukwambia usubiri processing ya mwezi mmoja, angalia ma benki, foleni hazieleweki na ukiuliza madirisha yenye matundu 7 wanaweka mhudumu mmoja au wawili, why? kwa sababu watanzania tumegeuzwa mamburukenge, kichwa cha wendawazimu na shamba la bibi, tukatae jamani