walibana sana,lkn nilijua iko siku wataachia....
kiko wapi..
lipumba kazi ni kwako hakikisha ccm wanaisha kusini
2015 utapata jawabu ,subiri kwanza tuipapatue katiba ya Chama Cha Mabepari.
Umesababishwa na Chama kilichopo madarakani ,ubepari wao sasa umetupia jicho kwenye machimbo ya gesi ,mkiendeleza kupokea vikofia vya manjano na shuka za kijani ,watawadidimiza kabisa ,vuzi kuendelea kuikataa CCM'mtafanikiwa...tatizo la watu wangu wa kusini ni umasikini.
Prof. Lipumba kunguruma Mtwara
NA MARIAM MAREGESI
9th October 2014
Aandaliwa mapokezi makubwa
Prof, Ibrahim Lipumba.
Baada ya serikali kutangaza kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara katika mikoa ya Kusini ya Mtwara na Lindi kwa takribani mwaka mmoja, Chama cha Wananchi (CUF) Mkoa wa Mtwara, kinafanya maandalizi ya kumpokea Mwenyekiti wa chama hicho, Prof, Ibrahim Lipumba, ambaye atafanya mikutano ya hadhara miwili mjini Mtwara.
Kiongozi huyo ambaye yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi, anatarajiwa kuwasili Mtwara mjini Oktoba 13, mwaka huu.
Akizungumza na NIPASHE katika ofisi za CUF mjini Mtwara, Katibu wa chama hicho mkoani humo, Said Kulaga, alisema anaandaa barua kwa ajili ya kuomba kibali polisi cha mapokezi ya kiongozi huyo.
Mwenyekiti (Lipumba) yupo katika mkoa wetu kwa ziara ya kikazi, tunaishukuru serikali kufungua mikutano, naandaa barua kwa ajili ya kuomba kibali kwa OCD cha kumpokea Mwenyekiti wetu, naamini tutakubaliwa kwa sababu tamko limetoka alisema na kuongeza:
Tutakuwa na mapokezi makubwa ya pikipiki, magari, bajaji pamoja na magari na yatakayoanzia Ghalani Mikindani saa 2:00 asubuhi na baadaye atazindua ofisi ya chama mkoa.
Alisema baada ya uzinduzi huo, Prof Lipumba atazindua matawi matatu ya chama hicho kabla ya kiongozi huyo kufanya mkutano wa adhara Ghalani Mikindani.
Kulaga, alisema siku ya pili ya ziara yake, Prof. Lipumba atakuwa na mkutano na viongozi wa CUF wa wilaya, jumuiya za kata na matawi yote ya chama hicho, na kisha atahutubia wananchi wa Mtwara mjini katika uwanja wa Mashujaa.
Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu Joseph Simbakali, alisema: Sina neno juu ya tamko hilo maana tayari serikali imetangaza kuruhusu mikutano na hakuna serikali mbili, alisema na kuongeza:
Mimi nitakupa maneno, lakini nimeazima ya Baba wa Taifa, uhuru wa kujitawala bila demokrasia ni udikiteta, lakini uhuru bila nidhamu ni fujo.
Alisema kuruhusiwa kwa mikutano hiyo isiwe mwanzo wa fujo, matusi na kejeli na kuonya kuwa endapo mtu atajihusisha na uvunjaji wa amani na kuleta vurugu sheria itachukua mkondo wake.
Na huko kwa "matajiri" mbona CCM imesambaa?? Watu wa hili jukwaa ni watu wa hovyo sana... kila siku wao hoja yao ni kwamba kusini na mikoa ya pwani ndio wachawi wa mabadiliko wakati huko bara kuna mikoa majimbo na kata zote zipo CCM na hawasemi! Kuna wapuuzi wanashindwa kabisa kufahamu kwamba wakati Lindi kuna wabunge wawili wa upinzani, Morogoro, Dodoma, Tabora, Ruvuma (naitaja hii coz' wengi wanapotaja kusini wanamaanisha Lindi na Mtwara); kote huko hakuna mbunge hata mmoja kutoka upinzani! Ukienda Iringa na Singida, kuna mbunge mmoja tu kutoka kila mkoa... lakini bado watu nongwa dhidi ya watu wa pwani na kusini haziwaashi... wanaona aibu kusema bayana kwamba hata bibi, babu, mama na baba zao ndio wanaoifanya CCM kuendelea kuwa madarakani!!!..tatizo la watu wangu wa kusini ni umasikini.