Elisha Gray alikuwa mtu wa kwanza kupata wazo la kusafirisha sauti kwenye waya (teknolojia ya simu) hata hivyo alizembea kuchukua hatua kwenda kusajili,kila siku alikuwa anaghairisha.Baada ya Muda Alexander Graham Bell naye akapata wazo na akaamua kuchukua hatua kwenda kulisajili.
Tarehe 14 February,1876 Alexander alienda ofisi ya usajili wazo (patent) akasajili na baada ya kughairisha kwa miaka mingi kumbe Elisha naye alienda ofisini siku hiyohiyo.Ila alipofika akaambiwa kuna mtu anaitwa alexander amekuja na kusajili saa moja lililopita hivyo hautaweza kuruhusiwa kulifanyia kazi.Akasema "mimi nilikuwa nalo tangu mwaka jana".Wakamjibu "Jambo kubwa sio kuwa na wazo jambo kubwa ni kuchukua HATUA".
Hadi leo dunia inamtambua Alexander Bell kama mgunduzi wa simu kwa sababu alichukua HATUA.
Ukiwa na wazo bila kuchukua hatua utashangaa wenzako wanasonga mbele wewe uko palepale.Wakati mwingine utashangaa unazungumzia wazo anakuja mwingine anafanya.MAWAZO HUWA HAYAKUSUBIRI,YAKIONA UNACHELEWA KUYATEKELEZA YANAENDA KWA MTU MWINGINE.
Je,Leo una wazo lolote ambalo umekuwa unaghairisha utaanza kulifanyia kazi?Share na wengine ili wasilalie mawazo yao wakaja kujilaumu mwishoni.
[HASHTAG]#TIMIZAMALENGOYAKO[/HASHTAG]