China yaionya Marekani

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
8,633
Reaction score
16,601
Waziri wa Ulinzi wa China aitahadharisha Marekani

Waziri wa Ulinzi wa China amesema kuwa ushindani wa nchi hiyo na Marekani umeingia katika nukta nyeti na hatari na kwamba China ni lazima iimarishe zaidi moyo wa kusimama imara.

Wei Fenghe ameyasema hayo kando ya kikao cha Kongresi ya Kitaifa ya Watu wa China mjini Beijing na kuchukua hatua ambayo si ya kawaida ya kuitaja kwa jina moja kwa moja Marekani kuhusiana na suala hilo na kuongeza kuwa, ni lazima kuimarishwa moyo wa mapambano na kusimama imara kwa ajili ya kuimarisha amani.

Waziri wa Ulinzi wa China ameongeza kwamba, Marekani inaiwekea mashinikizo China kupitia tuhuma za kuenea virusi vya Corona sambamba na kuiwekea vizuizi vingi, na kwa ajili hiyo Beijing ni lazima iimarishe moyo wa mapambano. Wei Fenghe amesema hayo baada ya hotuba ya Rais Xi Jinping wa China aliyelitaka jeshi la nchi hiyo kujiweka tayari kwa ajili ya vita. Marekani imekuwa ikiingilia masuala ya ndani ya eneo la Taiwan na Hong Kong, suala ambalo limekuwa likikosolewa vikali na China.

 
Ndio maana sasaivi wana wasiwasi mkubwa sana kuhusu China, walianza na Vikwazo dhidi ya Huawei, wakaja Corona na saivi wanadai China inapendelewa na WHO, hio inaonyesha wazi kuwa time inakaribia, sasaivi anachofanya marekani ni kama kutapatapa
Huu utawala wa Trump unaonyesha jinsi walivyoshindwa kupambana na China kiuchumi, intelijensia na teknolojia
 
Ndio maana sasaivi wana wasiwasi mkubwa sana kuhusu China, walianza na Vikwazo dhidi ya Huawei, wakaja Corona na saivi wanadai China inapendelewa na WHO, hio inaonyesha wazi kuwa time inakaribia, sasaivi anachofanya marekani ni kama kutapatapa
Ngoja wamarekani wa Nanjilinji waone komenti yako.😃😃
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…