Wadau naomba nianze kwa salamu. Kuna jambo la msingi ambalo nimeona nisipowashirikisha ni vibaya. Ni kuhusu harakati za CHASO Mkoa wa Morogoro. Wiki iliyopita ulifanyika uchaguzi uliowapatia majukumu viongozi wapya wa chaso.
Viongozi hao ni Ebenezer Kwayu (JONGEA MTANZANIA) anaetokea Mzumbe ambaye ndiye mwenyekiti wa Mkoa CHASO, Peter Manoti ambaye ni makamu na kamanda mwingine ambaye yeye ni Mwenezi.
Langu hapa jamvini ni moja tu, kwamba kwa nini kwa sasa CHADEMA Mkoa wa Morogoro wameamka kiasi ha kutisha tofauti na awali ambapo CCM walikuwa wakideka na kuliringia eneo hilo?..
Lakini pia viongozi waliochaguliwa kwa sasa wote uzoefu unaonesha ni wachapa kazi na wana Historia za kitaifa. Binafsi simpati sana Ebenezer Kwayu ila kama nakumbuka vizuri ni kamanda mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja. Hili utaliafiki utakapotembelea na kusoma makala zake ambazo huwa anaziandika kwenye gazeti la Tanzania Daima.
Lakini pia ni miongoni mwa waliokifufua chama chuoni mzumbe akiwa na kamanda ambaye kwa sasa amehitimu chuo (Matatizo).
Kwa upande mwingine, Manoti ni miongoni mwa wanaharakati waliosababisha wanafunzi elfu tatu Tanzania kupewa mkopo mwaka juzi baada ya kuandamana hata kabla ya kwenda chuo.
Ninapozitazama historia za hawa jamaaa napata hofu kwamba CCM watatambaje kama Morogoro ambacho ni kitovu chao imenyakuliwa kwa kasi ya ajabu.
Mbaya zaidi ni kwamba baada tu ya kuchaguliwa, makamanda hao waliapa kuwashughulikia CCM kwa kuwaita wakoloni weusi. na papo hapo vijana kumi na sita waliytangaza nia ya kugombea ubunge kwenye majimbo ya vigogo akiwemo Abood wa Morogoro mjini.
Tutafakari........