Habari wana jamvi
Nimejaribu kufatilia kwa nakala mbalimbali kuhusu faida na hasara za ujenzi wa kutumia interlocking bricks.
Sehemu nyingi naona zinaorodheshwa faida zake tu kama
- Urembo asilia
- Kupunguza mda wa ujenzi
- Kupunguza gharama za ujenzi kwani hakuna haja ya plaster wala skimming
- Thermal insulation
- Weight advantage (hizi tofali zinapunguza risk ya nyumba kutitia)
- Na kadharika...
Leo naomba tuachane kidogo faida zake. Ni wazi kwamba kila kitu kina faida na hasara zake.
Natamani kujua hasa changamoto za ujenzi wa interlocking bricks, na kama itawezekana kufanya assessment jinsi ya kutatua hizo changamoto.
Asanteni sana na karibuni