Changamoto ya akili msaada

Step by step

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2014
Posts
1,190
Reaction score
1,324
Habari wanabodi.

Nina hali flani ya kushtuka ninapopata taarifa ngeni, mwili unakosa nguvu, naharisha pia napata kichefchef hadi kutapika.
Badavya kuchek vipimo vingi nikaonekana niko sawa hivyo nikashauriwa kuonana na wataalam wa afya ya akili.

Dr wanasema ni ANXIETY hivyo wameniandikia dawa zifuatazo:-
1. Fluoxene mg20 1×1
2. Lorazepam 0.5mg ×1

Tangu nimeanza dawa wiki ya pili sasa sijaona unafuu maana asbh kichefchef na hali ya kutapika bado ipo pia mwili kukosa nguvu.

Naomba mwenye aliewahi tumia hizi dawa au kupitia hali kama yangu tupeane uzoefu
 
Hiyo hali mara nyingi nimeishuhudia kwa watu wanaopata misiba ya ghafla na wengine huzimia au kufariki kabisaa. Mara nyingi hiyo hali huisha yenyewe baada ya mtu kukubaliana na hali ama kupata faraja

Kama kwako ni tatizo la mara kwa mara pasipo kutegemea uzito wa tatizo. Bhasi ni kheri ukaenda kukutana na wataalamu
 
Me nikipqta taatifa mbaya ya kushtukiza huwa natapika,hata chakula hakipqndi tena
 
Chanzo ni taarifa hizo ulizozitaja, lakini pia inawezekana uko kwenye hali ya kuwa mwepesi kupata Anxiety/wasiwasi wa kupindukia upatapo taarifa hizo.

Anxiety pia huweza kuleta shida kwenye tumbo, kitu kiitwacho Irritable bowel syndrome, haya ni aina ya matumbo ambayo huathiriwa sana na hali ya vitu unavyoona, fikra, kusikia, kunusa na stress etc. Ambapo kuna mambo mengi huweza kujitokeza ikiwamo: kuharisha, kutapika, tumbo kujaa, kupitisha hewa kwa wingi etc.

Hii itahitaji mtu kukusikiliza tena na kuangalia dalili zako na mambo mengine.

Tiba ilihitaji kuhusisha pia:
1: Mwanasaikilojia
2: Dawa kulingana na hali husika na yaliyothibitika.
3: Mabadiliko kwenye aina ya vyakula
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…