Chamroho chamroho

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
CHAMROHO CHAMROHO.








1)Kapu lake mkononi,njiani ajizungusha.
Na mi mate i tumboni,usoni kajikausha.
Kwa mbali yu taabani,siri anasikitisha.
Chamroho chamroho,mate taka mdomoni.




2)mate yadondoka chini,mjengo kaupangisha.
Tama kuwa mjengoni,ndo mana ajivimbisha.
Hata kama ufipani,aende kulinganisha.
Chamroho chamroho,mate taka mdomoni.




3)msaliti yu mbioni,mradi ye kujirusha.
Tama chakulani,kala kabla kuivisha.
Kisa visa vya chumbani,za siri zisizoisha.
Chamroho chamroho,,mate taka mdomoni.





4)ka kifutu wa shimoni,magamba yamenza isha.
Atambaapo jangwani,nyayo zake aonyesha
Ila kweli yu moyoni,ataja kuwaangusha.
Chamroho chamroho,mate taka mdomoni.




5)vipi kifichwe jikoni,mpishi kabahatisha.
Ila kweli mfukoni,anataka bahatisha.
Mwisho mbaya katuni,kinyago ukijivishs
Chamroho chamroho,mate taka mdomoni.



Shairi:CHAMROHO CHAMROHO.
mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0655519736.
0765382386.
iddyallyninga@gmail.com
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…