Hatutaki VITA sisi..!
Ni bora CCM ituongoze hivi Maisha yote ila tukiwa na imani kuwa watoto wetu watakwenda Mashuleni salama na kurudi salama, hii ni pamoja na sisi Wazazi/Walezi kuwa na uhakika wa kurudi Majumbani kwetu salama, tukiwa tumepata ama tumekosa...
Chukulia mfano katika nchi ya Libya, tazama watu walivyo poteza Utu wao...! Tazama familia zilivyo potezana, yote haya yamekuwa ni chanzo/sababu ya kulazimisha Mageuzi pasipo kuwa na Mikakati thabiti.
Ni bora tule Dona la Dagaa ama Tembele tukiwa na Amani, kuliko kudondoshewa Boksi za Dawa na Pizza kutoka juu ya Ndege (msaada)
Kama bado vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama, vingali na Mapenzi na Utii kwa Chama, Upinzani usubiri Yesu arudi labda watafikiriwa kupewa Nchi waongoze.
Amani kwanza...Siasa baadae, No matter what..!