CHADEMA Iringa Mjini yazidi kupukutika

Hii hoja ya manunuzi ni kujaribu kujifariji kwakweli, haiwezekani watu woote hao wawe wamenunuliwa...ukinunua kundi kubwa hivyo la watu kutakuwa hakuna siri na ushahidi wa jambo hilo ungeshajulikana.
Msafara wa mamba na kenge wamo bendera kufata upepo ndani hao tumia misemo hiyo
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] nicheke miye jamani hao binadamu wa huko IRINGA walijivalisha lini huo uanachama wa CHADEMA hadi wajivue.

Lugha yenyewe peke yake inaashiria tabia mbaya ya umalaya unajivalisha kimya kimya unajivua mbele ya pesa za kununuliwa huo si ndio umalaya wenye hadhi ya ufuska kabisa.
 
Bila picha za hao watu 200 Uzi hauleti maana
 
Kama nakumbuka vile, kwamba ilishapigwa marufuku kuleta quote za gazeti la Uhuru hapa baada ya kugundua ni waongo kuliko hata shetani mwenyewe
 
Kwahiyo Iringa imepaa kimaendeleo, imepata viwanda vipya miambili, hongera Iringa kwa hatua ya maendeleo ya kiafrika.
 
Chakubanga alishapita huko na kifuko chake cha manunuzi
Ina maana makamanda ni kama karanga za diamond.
Wananunulika kirahisi hadi hasira.
Watu wa namna hii wangeuza nchi kirahisi sana.
 
Umaskini ni kikwazo kikubwa mno katika nchi nyingi za kiafrika katika harakati za kupigania demokrasia ya kweli.
 
Wamuulize yule mama na mwakalebela ndio watajua Rangi ya wajukuu Wa Mkwawa. Mosi hao madiwani wataonekana ni vituko mno mtaani mbili siasa za Iringa ni za ajabu mno kukugeuzia kibao ni sekunde tu.
 
Naona priority kwa sasa sio v wonder tena,ni kupata wanachama wapya kwa gharama yoyote ile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…