CCM, Rais Samia amechoka sifa zenu!

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,944
Watu waliongea sana.
Wengine tulithubutu kuandika....

"CCM Kila waziri, Mbunge na RC anasema Raisi Samia Kanituma"

Nikawauliza...Je ni lini na nyinyi mtaanza kutumia akili na vipaji vyenu kuwatumikia wananchi wa Tanzania?

Ni lini mtaanza kumsaidia Raisi katika utendaji kwa kila mmoja kuonyesha ubunifu wake pamoja na elimu zenu mnazotuonyesha kwenye CV zenu kubwa kubwa.
Wakati wa kutafuta ubunge huko majimboni.

Sasa Mama kaamua jana kuwaambia Live kwamba amechoka mapambio bali anataka mchape kazi.

Ameenda mbali kwa kusema mmemuachia zigo lote yeye...namnukuu

"Kila kitu Rais..kwani uraisi ni nini?..urais ni taasisi, mimi ni raisi ndiyo.lakini nyinyi ni wasaidizi na wawakilishi wangu hivyo ongeeni na wananchi"

Mwisho wa kunukuu.

Nadhani mlimuelewa vizuri kuanzia huko serikalini hadi huko kwenye Chama.

Tumieni nguvu,Busara na Weledi wenu kumsaidia mama.

Msije mkamsababishia pressure bure.

Nimewakilisha

commonmwananchi
10101.
 
walimsifia magufuli mwisho akaonekana lamana Hana magufuli wa watu wamwache mama wawatu
 
walimsifia magufuli mwisho akaonekana lamana Hana magufuli wa watu wamwache mama wawatu
Nidhamu ya uoga ni tatizo kubwa sana yaani kiongozi mwenye dhamana kama wazuri anaimba sifa badala ya kutimiza wajibu wake
 
Watu waliongea sana.
Wengine tulithubutu kuandika....

Anataka waongee na wananchi kwani wako madarakani kwa ridhaa ya wananchi? Yeye anapata watu kwenye hafla zake maana watu wanalipwa na makundi mengine kulazimishwa kutokea kwenye hafla zake, je wenzake wataweza vipi bila kuhonga wahudhuriaji?
 
Sukuma gang wanalia kilio cha mbwa koko
 
Hayo mambo ya rais katoa......, rais ametupa........, alianzisha yule mpuuuzi mpenda sifa
 
Bibi wa Taifa😁😁😁
Your browser is not able to display this video.
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…