youngsharo
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 2,491
- 500
Sio mzaha wala utani tena, sehemu kubwa ya makada wa CCM kwa sasa wameingiwa na wasi wasi mkubwa kabisa wa kushindwa kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu na kupoteza kiti cha urais kwa mara ya kwanza.
Hii imetokana na sababu zifuatazo.
1/Lawama na kutokuaminiana tena miongoni mwa makada wa CCM walioko kwenye timu za kampeni.
2/Upinzani mkali kutoka kwa wananchi dhidi ya mgombea urais wa CCM mahali anapopita kupiga kampeni.
3/Hamasa na Wingi mkubwa uliopo kwa watu wanaomuunga mkono Lowassa na UKAWA.
4/CCM kupoteza ngome zake zote za kisiasa hapa Tanzania(Pigo zito la Tanga limekuwa ndio hitimisho la kupoteza ngome zote).
5/Kushindwa kabisa kufanikiwa kuugeuza upepo mzito wa kutaka Mabadiliko kwa kutumia Propaganda mbalimbali.
Mtasubiri sanaaaa....IKULU hamwendi ng'ooo , TANZANIA bila CCM haiwezekani.
Ukawa Kweli mmekosa maono, mmebaki kulalamika na kushtaki ka watoto, jina UKAWA mwisho wa uchaguzi linakua UKIWA, Hapa kazi tuuiiiu
Mabadiliko
CHADEMA hawahutaji kufanya kampeni sana...kutushawishi wapiga kura....kwani kwa mtu aliyekaa hapa nchini na kupitia maisha magumu chini ya serikali ya CCM hiyo ni kampeni tosha na ni sababu tosha ya kuinyima kura CCM....
Wewe ndiyo muongo
Ndugu Mtanzania,
Usidanganyike hata kidogo.
Mabadiliko, Ni kaulimbiu iliyoanza kutumiwa tangu mwanzo wa kampeni za UKAWA, lakini imeanza kutumika vibaya na chama tawala [CCM] na wameibadilisha au kuiongeza chumvi eti mabadiliko ya kweli.
Sasa tujiulize je, si hawa wanaojitapa kila siku kuwa CCM ni ile ile?
Je, kaulimbiu yao si hapa kazi tu kwanini watumie mabadiliko ya kweli?
Kama mabadiliko ya katiba wameshindwa je, wataleta mabadiliko yapi? au badala ya twiga kupanda ndege sasa atapanda Bus?
Je, kati ya CCM na CHADEMA ni nani alikuwa wakwanza kudai mabadiliko? huyo ndo mwenye mabadiliko haswa maana ilikuwa ni dhamira yake kufanya mabadiliko lakini CCM wamesukumwa na nguvu ya wananchi ndio wanaodai mabadiliko.
Ni lazima tuwe wepesi wa kufikiri, hivi kweli Magufuli nae ni wakudai mabadiliko leo hii? ahahahahaa hata kama ndio watanzania ni malofa lakini bado hatujafikiwa kiwango hiki.
Mungu Ibariki Tanzania.
youngsharo
Wewe una ukweli gani? Zaidi ya propaganda
Viva ukawa
Lowasa ndo Rais wetu tushaamua ivo