Mwekezaji mwafrika tayari anafahamu na amezoea mazingira iliomo humu Afrika. Sikufahamu kwa nini mwekezaji wa hapa Afrika anahitaji waafrika wawe na tabia fulani kabla ya kuwekeza, maanake yeye ni mwafrika.
QUOTE]
sio kwa sababu mimi ni mwafrika na nazijua tabia za waafrika ndio niridhike na tabia hizo japo haziweki mazingira mazuri ya uwekezaji.
Kuna matatizo mengi ambayo wanakumbana nayo wawekezaji Waafrika ambao wangependelea tabia hizi zibadilike ili kazi zifanyike kwa ufanisi zaidi. Kuna tabia zilizokubuhu hasa kwa wafanyakazi vibarua (wenye elimu ya chini ambao hawafanyi kazi za maofisini)
Uchelewaji kazini: Hili suala kwa wafanyakazi wasio wa ofisini ni la kawaida sana, na japo limezoeleka, mwekezaji wa aina yoyote yule angependa mabadiliko.
Utoro kazini: Wafanyakazi hususan vibarua wanatabia ya kutoonekana kazini huku wakitoa sababu za mfano wa ‘safari ya ghafla kijijini', ‘kuna harusi ya mtoto wa shangazi', ‘niliamka tumbo linaniuma'
Kukosa umakini kazini: unaona kabisa mtu anafanya kazi ili imalize tu lakini sio kuhakikisha kuwa ameingiza juhudi zake zote kufanya kazi hiyo kuwa perfect.
na sababu nyengine nyingi ambazo ni kero kwa mwekezaji yoyote yule, haijalishi kama ni Mwafrika au mwekezaji mgeni.
kutokubali mapungufu yetu na kufanyia kazi kurekebisha ni moja ya sababu ambazo zimelazimisha Afrika ihitaji 'make-over'
btw ikiwa mwekezaji wa afrika tayari anajua tabia za waafrika na ana mazowea na ameridhika nazo kwa nini kuhitajike 'make-over'? kwa ajili ya nani?
ujumbe unaopatikana ni kuwa ama 'make-over' inatakiwa kufanyika ili kuridhisha muwekezaji wa kigeni, au wawekezaji wa afrika nao hawaridhi na hali iliyopo vile vile,