Arusha ( March 2012)
Nilikuwa nimetoka kupakia mawe mgodini nikapitia kijiweni kwa man kausi nikachukua shada misokoto minne nikatia kwenye buti la mgambo nililokuwa nimevaa, nikaanza safari kuelekea gheto.
Dakika mbili hazikupita wazee wa kazi wakafika wakaniuliza unatoka wapi? unaenda wapi na unaenda kufanya nini?
nikajaribu kujitetea lakini haikusaidia ukizingatia sikuwa tayari kutoa kitu kidogo. Wakaniambia twende kituoni nikagoma. Wakaanza kunishushia mkong'oto na virungu vyao huku wakinikokota, daah! nilimshukuru mungu nilivyofika kituoni.
Kufika kituoni wakaniandikia kesi ya wizi na uzururaji.
Nikavua mkanda wakanisachi wakaambulia 12500 tu na pakt mbili za kondom mfukoni.
Wakaniambia nivue viatu huenda nimeficha vitu vingine kwenye viatu.
Ile kutoa tu kiatu cha kwanza mbwa wa polisi aliyekuwa hapo akakimbia, yule afande aliyekuwa kaunta akaanza kutapika maafande walionikamata wakaniambia basi nenda ukavulie huko chooni, hilo buti lilikuwa na miezi miwili halijafuliwa harufu iliyokuwa inatema...