Burudani Ama miracle ya neno "ADJUST"

Judgement

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2011
Posts
10,326
Reaction score
4,789
Ninajua wengi wenu mlishawahi kusikia neno hili , ambavyo ndugu zetu hasa wa kutoka mkoa wa Kilimanjaro , walivyokua wakilitumia neno "Adjust" kwa fujo ku'cover maeneo mengi ya maneno mengine .

Nimeona si vibaya kwa waliokwisha lisikia tukajikumbusha , na nna imani hawatakosa baadhi ya Members ambao hawajawahi kukisikia hiki nikisemacho .

Mf. Wake ni kama hivi : -
"Si unamjua yule mshkaji wangu ambae hua tunaendaga nae Ku'ADJUST ?
Alini'ADJUSTIA call kwamba atanipitia tuka'ADJUST.
Midamida akaja tuka'JIADJUST kwenye ndinga yake tukaondoka.
Kufika pale kwenye mataa (trafic light) zikawa taa nyekundu hazi'ADJUST namie nna kiu balaa ya kuwahi kua'ADJUST laga Babaangu .
Nikamwambia mshkaji aa'ADJUST kwa pembeni , aka'ADJUST tukapita .
Mara tukafika Bar, chapchap tukamwambia muhudumu atu'ADJUSTIE , aka'ADJUST .
Tukaanza kua'ADJUST keroro , tuka'ADJUST , tuka'ADJUST, gafla mie nikaskia tumbo la kua'ADJUST (Kuharisha) lina nia'ADJUST.
Ikabidi niende toilet nika'ADJUST. Kufika toilet naskuma mlango , kumbe kuna mtu nae ana'ADJUST.
Si ndiyo ikabidi nitafute chocho nika'ADJUST.
Nikakuta kakichaka nikaanza kua'ADJUST.
Nime'ADJUST, nime'ADJUST.
Namaliza ku'ADJUST , kumbe sina maji ya kuji'ADJUSTIA .
Ikabidi niji'ADJUST na majani .
Mamah yangu! Kumbe ni majani ya kuwasha ,
Aacha yaanze kuni'ADJUST !
Yanani'ADJUST na mie naji'ADJUST kwa kujikuna .
Kwaheri naona usingizi unani'ADJUST.
 
hizi msejei shem..au ni katika kumalizia bundle!???hehehehe

mimi adjust nimeiskia sana kwenye daladala, "hebu ADJUST kidogo tukae wawili hapo"

au konda, "mama ADJUST kidogo hapo muingie wote, jioni hii kila mtu anwahi nyumbani."

"abiria ADJUST tuenee wote, tupendane jamani."
 

Shem za masiku? Umeona eeh!
ADJUST inavyochomekwa maeneo kibao , na haimsumbui aambiwae uelewa nini anatakiwa akifanye !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…