Breaking From the Past

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
16,105
Reaction score
40,777
Habari za asubuhi wanajamii.

Katika tafakari zangu za maisha, niliwahi kutamani kuwa mwanasiasa. Lengo kuu lilikua niwanie nafasi ya juu kabisa ya uongozi katika nchi yangu Tanzania. Sababu kubwa iliyokua inanisukuma ni kuona utajiri mwingi wa mali asili na vivutio vya utalii pamoja na watu wa kutosha wenye ueledi, lakini bado nchi yangu iko kwenye dimbwi la umasikini.

Nikajiuliza sana matatizo ya nchi yangu ni yapi, nikajaribu kufanya tafiti ndogo ndogo na kupata mawazo mbadala kutoka kwa wanazuoni na watu halisi wa kawaida kabisa. Baada ya kupata mawazo hayo chanya, nikachanganya na akili zangu (kama alivyotushauri Raisi mstaafu) nikagundua nchi yetu imebanwa na mambo yafuatayo:

1. Unafki wa kupitiliza;
2. Siasa zinaendeshwa na kuongozwa na watu wasio na asili ya uongozi na watu wasio wawekezaji yaani hawana mali zisizo hamishika (madalali wa tumbo na hawana cha kupoteza);
3. Wananchi wa nchi yangu wanapenda kubakia kwenye comfort zone yao, hawapendi mabadiliko;na
4. Siasa za vyama zinachukuliwa kama dini, watu hawako objective.

Baada ya kubaini hayo, sasa nimekua ni mtu ambaye ninaye amini kwenye ku-break from the past. Kuzalisha Tanzania mpya yenye mentality mpya na namna mpya ya kushughulika na mambo yake.

1. Tunahitaji kiongozi atakayeendesha nchi yetu kwa kujitoa ufahamu na kufanya maamuzi magumu (kama anavyofanya Muheshimiwa Raisi Magufuli);
2. Tuache kuendesha nchi kwakutumia election manifestos za vyama vya siasa, tunahitaji kuwa na sera za nchi zitakazo ongoza maendeleo yetu ya kiuchumi na mahusiano yetu ya kimataifa sera hizi ziwe kwenye katiba. Hii itatusaidia kuondokana na mabadiliko ya kimifumo pale chama kingine kitakapochukua nchi;
3. Kuchochea utaifa (patriotism) kwa kuwa na programs na propaganda zitakazo saidi kukuza na kusimika utaifa kwa watoto wetu;
4. kupeleka raia wetu nje ya nchi ili kuongeza exposure na kupunguza ushamba; na
5. Kuondoa alama dhaifu kwenye nembo ya taifa kama vile twiga na kusimika alama zinazoonyesha ujasiri kama vile mamba au papa wa majini.

Kwakua mpaka sasa sijawahi kujiunga na chama chochote cha siasa, na huyu muheshimiwa anaweza akakaa madarakani kwa miaka zaidi ya kumi(kama ilivyopendekezwa na mzee ruksa)
basi si vyema nika share mawazo yangu na nyinyi wanajamii. Kwani sina nia ya kuwania hiyo nafasi tena, naendelea na maandalizi yangu ya maisha ya uzeeni. Asanteni kwa kusoma.
 
Fikiria jinsi ya kusaidia watanzania nje ya siasa.

Mana watanzania tunaongea sana kuliko kutenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…