Bomu Laua Watu 12

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,007
Reaction score
168,592
Habari kutoka Somalia zasema mshambuliaji wa kujitoa muhanga amejilipua ndani ya gari na kuwauwa watu 12 na kujeruhi wengine wanane. Mlipuko huo umetokea nje ya makao makuu ya maafisa wa usalama .

Mwandishi wa BBC anasema kuwa waliofariki ni maafisa usalama na wengine raia wa kawaida waliokuwa katika mkahawa karibu na hapo. Kumekuwa na ongezeko la mashambulizi huku vikosi vya nchi hiyo vikipambana na wanamgambo wa al shaabab.
 
Huko mambo ni magumu. Lakini ni wazi kuwa nguvu za Al Shaabab zimepungua sana na zitazidi kupungua zaidi. Kuwamaliza kabisa ni ngumu - ni mchakato utakaochukua muda mrefu na kutakuwa na wahanga wengi wa matukio yao ya kigaidi. Jumuia ya Kimataifa inatakiwa kuendelea kutoa msaada wa hali na mali kwa serikali ya Somalia ili kuimarisha vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama (Jeshi, Polisi, Usalama wa Taifa, n.k). Wamarekani waendelee kurusha "drones" ili kubaini maficho ya waliobakia na kikubwa zaidi, waendelee kuwasaka viongozi wao kwa udi na uvumba popote walipo duniani. Mwisho wao utafika tu!
 
Hawa Al Shabab ni hatari sana, tuombe Mungu yasitukute.
 
hawa jamaa ni hatari sana wapigwe vita kwa nguvu zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…