engmtolera
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,149
- 1,441
bangi mbaya ndugu yangu.
🤣🤣Boban wa pili kushoto.
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba, Haruna Moshi Boban jana alikuwa kivutio kwa mashabiki, wasindikizaji na hata baadhi ya wasafiri waliomuona wakati wakiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, kuelekea Sudan. Uvaaji wa Boban, ndio uliowavutia watu kumtizama, kutokana na kuvaa kama mtu asiyesafiri.
Boban alikuwa amevaa fulana, suruali ya kimichezo trakisuti na kandambili, hivyo kusababisha watu kuvutika kumuangalia, huku baadhi yao wakibaki kujiuliza kuhusu vituko vya nyota huyo ambaye mashabiki humuita Balotteli wa Bongo.
Morogoro kuna Fathet pekupeku kokote aendako hutembea peku, hutumia pia baiskeli, (Anita)Mbona hata mie hupendelea kuvaa sandals zozote zitazokuepo around ili kuepa longolongo za kuvua na kuvaa viatu. Ni mapenzi tu ya mtu.
BTW, there is only one Boban, Zvonimir Boban, left-footed na kiungo mpishi mahiri kabisa wa zamani wa Dinamo Zagreb, Milan 1899 na timu ya taifa Croatia, hao wengine wa kwenu ni wakuchonga tu si lolote si chochote...they don't worth the comparison.