Well saidNikiri kuwa nimekuwa mpenzi wa BM Coach kwa muda mrefu sasa ila hili la safari hii limeanza kunichefua.
Alhamisi ya tarehe 07/09/2023 nilisafiri na basi la 1.30 asubuhi. Mshangao wa kwanza ni kutokuta basi nililoahidiwa kwenye tiketi kwa kiwango cha nauli. Nilikata basi la 40,000 likaja la 37,000. Wakaomba radhi wakaturudishia 3,000 tukapotezea.
Kurudi 10/09/ 2023 Basi linalopita moshi saa 3 asubuhi jambo lile likajirudia bila hata samahani. KIBAYA ZAIDI HATA CHENJI YEU HATUKUPEWA. Hatujui ni mmiliki/meneja/ au konda aliyepita na chenji yetu. MZEE ANGALIA WATU WAKO. Namba zetu wanazo. Watupe chenji zetu.
Jambo lingine baya ni kuanza kujaza watu. Haswa hapo mbele....tukiwauliza mara oo ndugu wa askari, mara oo staff...haina hata maana kukata siti za mbele... unaishia kuangalia vichogo vya watu.
Lililonitia shaka ni hii biashara ya vifurushi pori anavyopewa konda kabla ya kuondoka na watu wanaomsubiri njiani kumpa na kupokea.... MZEE BM angalia magari yako yasigeuzwe punda wa unga.... vifurushi vipite ofisini. Waache njaa.
La mwisho. Simu za madereva. Ni nyingiiiiii. Kusogoa njia nzima. Wapunguze...ndio zibaki zile muhimu na zingine awaambie tu , nadrive...niakupigia... watu watakuja pokea simu za msiba watubwage....ohooo...
Au mpaka tupeleke ushahidi LATRA? Ya nini yote hayo?
Panda MaranguNikiri kuwa nimekuwa mpenzi wa BM Coach kwa muda mrefu sasa ila hili la safari hii limeanza kunichefua.

mabus mengi yana hii keroSimu za madereva. Ni nyingiiiiii. Kusogoa njia nzima
Unapoona apungufu kwenye biashara ya mwenzio sema ili arekebishe/aboreshe. Utafanya biashara ngapi?Ni fursa kwako kuanzisha kampuni bora ya usafirishaji ambayo haitakuwa na kasoro pia utapata wateja wengi.
Mimi kwenye basi sifuati U luxury bali kufikq nako enda,Hakuna cha luxury kwenye basi ni usanii mtupuUsiombe Ukate Luxury Ac inazimwa ukiombwa Iwashe Utaskia wewe Nyumbani kwako kuna Ac.
Ni fursa kwako kuanzisha kampuni bora ya usafirishaji ambayo haitakuwa na kasoro pia utapata wateja wengi.
Mkuu yapo mabasi siku ukipanda utajua ukweli kuwa yapo mabasi wakati wengine wanalipisha elfu 40 wengine hata elfu 25 unaenda ila unyamaze....mpaka vigoda vipo. Haachi mtu.Mimi kwenye basi sifuati U luxury bali kufikq nako enda,Hakuna cha luxury kwenye basi ni usanii mtupu
Nashukuru kwa pole. Private ninazo ila swala la upaikanaji wa mafua bora mafuta lilinisukuma kwenye public. Pia sikuwa na uharaka wa safari.ukitaka usisumbumbuke kwenye hizi huduma za "public" hakikisha umepata "private"
tunaishi katika ulimwengu wa tatu, mambo ni mengi.
anyway, pole kwa usumbufu mkuu!
Huyu jamaa ni lofaHuyu ndiyo mswahili sasa, hajali thamani ya fedha na huduma unayolipia!! Anakwambia kaanzishe kampuni yako sijui tutaelimika lini kwenye swala la kuboresha huduma!!
Kwa hiyo nchi ikiwa na matatizo anzishe nchi yake?Ni fursa kwako kuanzisha kampuni bora ya usafirishaji ambayo haitakuwa na kasoro pia utapata wateja wengi.