Si kwa Tanzania beef zetu tz ni kuwachukia wale waliofanikiwa, na wengine wanathubutu kutengeneza nao beef ili warudi kwenye gemu kwa kumchafua mwenzake ambacho si kitu kizuri. Mi napendaga zile beef za mwenzetu za kutengeneza mkwanja kama Kanye West na 50, beef yao ya kubust mauzo ya album zao ndio beef nzuri, sio zile beef zetu za kuponda hata kama mtu anafanya vizuri sana au kumshusha mmoja mwengine apande au kisa eti jamaa anaringa, ana nyodo, anajisikia ila ukija kuchunguza ni wivu tu. Beef zetu hasa za miaka hii za hawa watu wawili zinaua mziki kwani wanaangaliwa wao, wengine hawatazamwi, japokuwa mmoja anamtegemea sana mwenzake na kila siku anaomba mungu amuweka hai ili aendelea kushine kupitia yy.